Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Saudi Arabia Mheshimiwa Eng. Zena Ahmed Said amesilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia anayeshughulikia masuala ya Itifaki, Mheshimiwa Abdulmajeed R. Alsmari. Balozi Eng. Zena aliwasilisha hati hizo tarehe 19 Mei 2026 kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia zilizopo jijini Riyadh. Mara baada ya kuwasilisha Hati, Balozi Zena alifanya mazungumzo na Mhe. Alsmari ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabia. Kwa upande wake Waziri Alsmari alimtakia Balozi Zena uwakilishi nzuri na wenye mafanikio kwa kipindi chote cha uwakilishi wake nchini Saudi Arabia.