Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mheshimiwa Dkt. Moh'd Juma Abdalla awasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia anayeshughulikia masuala ya Itifaki, Mheshimiwa Abdulmajeed R. Alsmari. Balozi Dkt. Moh'd aliwasilisha Hati hizo tarehe 17 Oktoba 2023 alipofika kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia zilizopo jijini Riyadh, Saudi Arabia. Mara baada ya kuwasilisha Hati, Balozi Dkt. Moh'd alifanya mazungumzo na Mhe. Alsmari na kuahidi kuwa Ubalozi utaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabia. Naye Waziri Alsmari alimtakia Balozi Moh'd uwakilishi mzuri na wenye mafanikio kwa kipindi chote cha uwakilishi wake nchini Saudi Arabia.