Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan awasili nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa Kilele wa Saudi Arabia na Nchi za Afrika uliofanyika tarehe 10 Novemba 2023 jijini Riyadh. Mkutano huo wa siku moja ulilenga kujadili masuala ya ushirikinao kwenye sekta za biashara, uwekezaji, utalii, kilimo, nishati na madini. 

Katika zaira hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakiwemo Mawaziri na Viongozi Waandamizi wa Serikali, ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, inayokusudia kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii. Mheshimiwa Januari Yusuf Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikuwa ni miongozni mwa Mawaziri waliombatana na Mheshimwa Rais.