Mhe. Anthony Peter Mavunde, Waziri wa Madini aliwasili nchini Saudi Arabia na ujumbe wake wa watu watano (5) kuhudhuria Mkutano wa nne (4) wa Madini uliofanyika jijini Riyad - Saudi Arabia tarehe 8 hadi 12 Januari 2024. Ujumbe wa Mhe. Waziri pia ulipata fursa kutembelea maonesho ya Madini yaliyofanyika sambamba na Mkutano huo.